Tatizo la unene limeongezeka kwa
kasi kwa vijana wa vijijini nchini China, utafiti uliofanywa umebaini
na kuonya kuwa hali hiyo inachangiwa mabadiliko ya uchumi wa jamii.
Takwimu za utafiti huo
zilizochukuliwa kutoka kwa tafiti sita za serikali ya China kwa
wanafunzi kwenye shule za vijijini huko Shandong wenye umri wa
kuanzia miaka 7 hadi 18.
Asilimia za watoto wenye uzito
mkubwa nayo imeongezeka kutoka asilimia 0.7 hadi asilimia 16.4 kwa
watoto wakiume na asilimia 1.5 hadi asilimia 14 kwa watoto wakike.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni