Tetemeko lenye nguvu kubwa lililofikia kipimo cha
alama 7.8 limeuwa watu 41 nchini Ecuador, Makamu wa rais wa nchi
hiyo, Jorge Glas amesema.
Tetemeko hilo limetokea jana karibu na mji wa
pwani ya kusini wa Muisne, na kusababisha madhara makubwa katika
maeneo mengi.
Hali ya hatari imetangazwa katika mikoa sita na
jeshi la kulinda taifa limeitwa kusaidia zoezi la uokoaji.
Waokoaji wakiwa juu ya vifusi wakijaribu kutafuta watu waliofukiwa
Vikosi vya uokoaji vikiendelea na zoezi la uokoaji
Wagonjwa na ndugu zao wakiwa nje ya Kliniki ya Colombia baada ya kutakiwa kutoka nje kufuatia tetemeko hilo
Watu wakiwa hawaamini kilichotokea baada ya tetemeko kuleta madhara makubwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni