.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 4 Aprili 2016

TIMU YA TANESCO YAICHAPA QIBLATEN

Mkuu wa wilaya ya Iringa. Richard Kasesela ( kulia ) akiongozwa kwenda kuzikagua timu za Tanesco na Qiblaten kabla ya kuanza kwa pambano lao. 

Timu ya Tanesco imeifunga timu ya Qiblaten kwa bao 1-0 na kutwaa kombe la Hyperlink na zawadi nono ya Ng'ombe na mshinid wa pili Qiblaten kupata zawadi ya Mbuzi. 

Mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ambaye aliwashukuru Hyperlink kwa kufufua mchezo wa mpira wa miguu. 

Timu zilizo shiriki zilikuwa 10. Mdhamini na mwandaaji wa mashindano hayo Bwana George Fuime ameomba wilaya ifufue viwanja na kuendelea kubariki mashindano. 

Naye Mkuu wa wilaya hiyo aliahidi kuendelea kuzijenga timu kama Lipuli na African Wonderers hasa kwa kuwatafutia wadhamini, lakini pia ikiwezekana wapatikane wabia ambao watanunua timu hizo na kuziendesha kitaalamu. ​
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitambul;ishwa kwa waamuzi wa pambano hilo
                 Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akifuatilia pambano hilo



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni