.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 11 Aprili 2016

UKATILI WA KINSIA SOKO LA TABATA MUSLIM JIJINI DAR ES SALAAM WAPUNGUA KWA MSAADA WA SHIRIKA LA EfG.

Msaidizi wa kisheria katika soko la Tabata Muslim, Aisha Juma akizungumza wakati akifungua tamasha la kuongezea uelewa kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia masokoni lililofanyika mwishoni mwa wiki Soko la Tabata Muslim jijidi Dar es Salaam ambapo ilielezwa kupungua kwa vitendo vya ukatili katika soko hilo. Upunguaji wa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia umetokana na elimu iliyotolewa na wasaidizi hao wa kisheria kwa msaada wa Shirika la Equality for Growth (EfG)
 Msaidizi wa kisheria katika soko hilo, Irene Daniel akielezea kupungua kwa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo kutokana na msaada wa wasaidizi hao wa kisheria masokoni waliowezeshwa na Shirika la EfG.
 Msaidi wa kisheria katika soko hilo akichangia jambo.
 Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la EfG, Mr Shabani akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya ukatili wa kijinsia masokoni.
 Wasanii wa Kundi la Machozi lenye maskani yake Temeke jijini Dar es Salaam wakitoa burudani kwenye tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki viwanja vya Soko la Tabata Muslim.
 Burudani zikiendelea katika viwanja hivyo.
 Mpiga picha wa EfG akipiga mzigo katika tamasha hilo.
Watoto nao walikuwepo kushuhudia burudani za tamasha hilo.
 Katibu wa Soko hilo, John Nombo (kushoto), akichangia jambo kwenye tamasha hilo. Kulia ni Mratibu wa Tamsha hilo,Bibi Grace kutoka Shirika la EfG.
 Baunsa wa kujitolea wa Tamasha hilo naye alishindwa kuvumilia midundo ya ngoma iliyokuwa ikitolewa na kundi la Machozi ambapo alijikuta akiingia uwanjani naye kufanya vitu vyake kama anavyoonekana.
 Wananchi wakifuatilia tamasha hilo.
Mkazi wa Tabata, Mwahija Rajab akichangia jambo kuhusu ukatili wa kijinsia.
Burudani kutoka kundi la machozi zikiendelea.
 Taswira ya jukwaa kuu katika tamasha hilo.
Wageni waalikwa na wasaidizi wa kisheria katika soko hilo na viongozi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), wakiwa katika picha ya pamoja.
 
 (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni