Timu ya Manchester United ya vijana
wa umri chini ya miaka 21, imetwa tena taji la Ligi Kuu ya Uingereza
kwa umri huo baada ya kuifunha Tottenham katika dimba la White Hart
Lane kwa magoli 3-2.
Kwa ushindi huo kikosi hicho cha
kocha Warren Joyce, kimeweka historia ya kutwaa kombe hilo mara tatu
katika miaka minne, ambapo katika mchezo wa jana magoli ya Manchester
United yalifungwa na Andreas Pereira, Donald Love na Guillermo
Varela.
Donald Love akiachia shuti lililojaa wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni