.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 4 Mei 2016

ATLETICO MADRID YATINGA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA KWA MARA YA PILI MFULULIZO


Timu ya Atletico Madrid imetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo ndani ya miaka mitatu kwa kuiengua Bayern Munich kwa goli la ugenini katika mchezo wa nusu fainali uliokuwa na ushindani mkali jana usiku.

Ikiwa ipo nyuma kwa goli moja walilofungwa katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, Bayern walisawazisha kupitia kwa mpira wa adhabu wa Xabi Alonso, ambapo pia Kipa wa Atletico Jan Oblak aliokoa penati ya Thomas Muller.

Mchezaji Antoine Griezmann aliisawazishia Atletico, hata hivyo baadaye goli la kichwa la Robert Lewandowski lilifanya hali kubadilika. Nafasi ya Atletico kupata goli la pili ilipotea baada ya Fernando Torres kukosa penati.
                       Robert Lewandowski akipiga mpira wa kichwa uliojaa wavuni 
                           Fernando Torres akipiga penati iliyopanguliwa na kipa Neuer 
             Wachezaji wa Bayern Munich wakitoka vichwa chini baada ya kutolewa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni