.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 15 Mei 2016

BOMU FEKI LAHAIRISHA MCHEZO WA MAN UTD NA BOURNEMOUTH

Hali ya taharuki imetokea katika uwanja wa Old Trafford wakati simu ya mkononi iliyofungwa waya ilipokutwa ikiwa imetelekezwa chooni kabla ya kuanza kwa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Uingereza baina ya Manchester United na Bournemouth.

Mchezo huo ulilazimika kucheleweshwa kunaza kufuatia tukio hilo la bomu feki, na baadaye polisi kushauri uhairishwe kabisa, ambapo maafisa usalama walilazimika kusimamia zoezi la mashabiki kutoka nje.

Timu ya kutengua mabomu iliitwa kuchunguza kifaa hicho kwa kutumia mtambo wa roboti wa kutengua mabomu, pia mbwa wa kunusa milipuko walitumika kufanya upekuzi katika maeneo yote ya uwanja huo.
                           Polisi akiwa na mbwa wa kunusa milipuko wakifanya upekuzi
                          Polisi akifungua pochi iliyoachwa uwanjani na shabiki wa mpira
                           Mashabiki wakitoka nje ya uwanja baada ya tishio la bomu feki

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni