Mkuu wa Wilaya Iringa, Mh Richard Kasesela alifunga mafunzo ya "Kungfu" yalikuwa yanaendeshwa na SHOKINJI KEMPO.
Washiriki kutoka Dares salaam na Dodoma walionyeshana ufundi wa kung Fu na wengine walipandishwa madaraja.
Katika hotuba yake aliwaomba Kemp hiyo kuwa walinzi wa amani kwani sifa kubwa ya wacheza kungfu ni kuhakikisha amani. Mwanzilishi wa Shokinji Kemp alifariki tarehe 14 mwezi wa 5 miaka 60 iliyopita huko Japan.
Mwenyeji wa masjhindano hayo Diwani wa Kitanzini ambaye yupo daraja la juu (Mkanda mweusi) alishukuru sana uwepo wa Mkuu wa wilaya na kuahidi kumsadia katika kulete amani na utulivu pamoja na kuzuia vijana kuingia kwenye tabia mbaya za uvutaji bangi na ulevi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni