Mkuu
wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk.
Reginald Mengi (hayupo pichani) kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo
vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya
mbinu za kiusalama chuoni hapo.

Mwenyekiti
Mtendaji wa Makapuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki
wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa
muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama
wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama (hawapo pichani)
katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es
Salaam Mei 16, 2016.

Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya
Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu
nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa
washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa
kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akitoa historia fupi ya chuo hicho kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akiagana na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed (kulia) mara baada ya kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama (hawapo pichani) katika chuo hicho kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa mbele wa Jengo la Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
IMELEZWA
jukumu la ulinzi na usalama kwa dunia ya sasa halimo kwenye mikono ya
polisi na wanajeshi pekee bali ni la kila mtu katika nafasi aliyopo kama
amani na demokrasia inatakiwa kuendelea kuwapo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed wakati akizungumza na Modewjiblog ofisini kwake baada ya mhadhahara ulioshirikisha wataalamu wa masuala ya habari kutoka sekta binafsi na umma ambao wanachukua kozi ya mbinu za usalama chuoni hapo.
“Zamani mambo ya usalama yalikuwa ya wanajeshi na Polisi lakini kwasasa mambo ni tofauti, kila mmoja anatakiwa kuhakikisha anakuwa mlinzi ili uwepo usalama wa kutosha kwahiyo tunaamini washiriki wakirudi vituoni kwao watazingatia usalama.
“Wote wanaokuja hapa wanakuwa ni viongozi au viongozi watarajiwa na kama sasa tuna wanafunzi 38, 12 sio Watanzania ni kutoka Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Namibia, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Nigeria na China,” aliongeza Meja Jenerali Mohamed.
Wataalamu walioendesha mihadhara hiyo ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi ambaye amepata nafasi ya kutoa elimu kuhusu habari kwa sekta binafsi na Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC) na mwanazuoni Dk. Ayoub Rioba ambaye aliwasilisha sekta ya umma.
Akielezea ujio wa Dk. Mengi chuoni hapo, alisema wamekuwa na taratibu wa kukaribisha watu mbalimbali ambao wanawaona wana uwezo wa kuelezea uzoefu wao katika mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa na faida kwa washirika.
Alisema chuo chao kimekuwa hakina walimu wa kudumu hivyo pamoja na kutumia watu mbalimbali kama walivyofanya kwa Dk. Mengi pia wamekuwa wakiwatumia walimu wa vyuo vikuu ili kutoa elimu ambayo itawasaidia washiriki katika masomo yao ambayo wanayapata chuoni hapo.

“Chuo
chetu hakina walimu wa moja kwa moja kwahiyo huwa tunatumia walimu
kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini lakini pia huwa tunakaribisha watu
maarufu wanakuja ku’share’ uwezo wao kwa washiriki ambao wanakuwa wapo
masomoni.
“Dk. Mengi ameshafika hapa chuoni mara tatu na sio mtu wa kwanza kuja alishakuja Pius Msekwa, Mawaziri, Katibu Mkuu kiongozi na hata jana tulikuwa na (Dkt. Ayoub) Rioba,” alisema Meja Jenerali Mohamed.

Alisema
chuo hicho hupokea washiriki ambao ni viongozi katika ofisi
wanazofanyia kazi na hupokea washiriki kutoka nchi mbalimbali ambapo
hupatiwa elimu kuhusu usalama ili wanapotoka chuoni hapo wakafanye kazi
kwa umakini ili wasiweze kuwa sababu ya kupoteza usalama katika maeneo
yanayowazunguka.
Katika mada yake iliyozungumza kuhusu wajibu wa vyombo vya habari binafsi katika usalama wa Taifa, Dk. Mengi alisema vyombo visipokuwa makini vikawajibika kitaaluma vinaweza kusababisha migogoro itakayohatarisha usalama wa taifa.
Akielezea uzoefu wake kama mmiliki wa vyombo vya habari binafsi alisema usalama ni jambo la muhimu kwa kila mtu bila kujali ana nafasi gani katika nchi hivyo ni wajibu wa kila mtu kushiriki katika kuimarisha usalama.
Alisema vyombo vya habari wanahakikisha habari zinazotolewa zinakuwa hazina madhara ambayo yanaweza kusababisha upotevu wa amani lakini kusimamia misingi na maadili ya uandishi wa habari.

“Kama
kuna utulivu, mshikamano na usalama wa taifa kuna faida kwa taifa na
hilo linaweza kusaidia kukuza kwa uchumi wa nchi ambao pia utakuwa na
faida kwa kila mwananchi, “Vyombo vya habari vinatakiwa kufuata maadili
ya kazi yake kuupasha umma habari na kutoa elimu bila kuathiri hali ya
amani na utulivu kwa sababu tunaelewa kuwa pamoja na kutoa habari lakini
pia ni wajibu wetu kuhakikisha kuna usalama nchini,” alisema Dk. Mengi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni