.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 3 Mei 2016

EDEN HAZARD AWAPATIA UBINGWA WA UINGEREZA TIMU YA LEICESTER CITY


Timu ya Leicester City imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza na kuweka historia kubwa ya mchezo wa soka nchini humo.

Ushindi huo umetokana na Tottenham kutoa sare ya magoli 2-2 na Chelsea jana usiku, na kusaidia kuipatia mafanikio timu hiyo inayonolewa na kocha Claudio Ranieri.

Leicester City ilianza kampeni ya kuwania taji hilo katika msimu huu kwa mafanikio baada ya kunusurika kushuka daraja katika msimu uliopita.
Mashabiki wa Leicester City wakishangilia ubingwa baada ya Chelsea kutoa sare na Tottenham
                       Eden Hazard akipiga mpira uliozaa goli la kusawazisha la Chelsea
 Mpira uliopigwa na Eden Hazard ukitinga wavuni huku kipa wa Tottenham akishindwa kuuzuia



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni