Miili ya wapanda milima wawili
Wamarekani imepatikana kwenye eneo la theluji katika mlima wa
Himalaya ikiwa ni miaka 16 kupita tangu wauwawe na maporomoko ya
makubwa theluji.
Mpanda milima maarufu duniani, Alex
Lowe, alikuwa amepanda umbali wa mita 8,013 katika kilele cha
Shishapangma huko Tibet Oktoba 1999, akiwa na mpiga picha wake David
Bridges walipokumbwa na maporomoko hayo ya theluji.
Alex Lowe na David Bridges
wamepatikana wiki iliyopita miili yao ikiwa bado imefunikwa na
theluji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni