Muwania urais wa Republican
anayeongoza, Bw. Donald Trump, ameituhumu China kwa 'kuibaka'
Marekani, ikiwa ni muendelezo wa kurejea kauli zake za kuikosoa China
dhidi ya sera zake za biashara.
Bw. Trump ambaye ni mfanyabiashara
bilionea amewaambia watu waliofika kwenye mkutano wake wa Indiana
kuwa China inahusika na wizi mkubwa katika historia duniani.
Bilionea huyo kwa muda mrefu amekuwa
akiituhuma China, kwa kucheza na fedha yake ili kuzifanya bidhaa za
nchi hiyo kuwa na unafuu katika soko la dunia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni