Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alikutana na wazazi na walimu wa shule ya sekondari Mkwawa na kukagua ujenzi wa maabara unaenedela katika shule hiyo. Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya aliongozana na afisa tarafa wa Manispaa ya Iringa Bwana Bujo Mwakatobe.
Akizungumza na wazazi na walimu wa shule ya sekondari Mkwawa Mh Kasesela alisikitishwa sana na kuporomoka kwa elimu katika shule hiyo. Shule ya Mkwawa imekuwa ya 24 kati ya shule 25 zilizopo manispaa, na kimkoa ni ya 101 kati ya shule 131 ambapo kitaifa ni ya 1199 kati ya shule 3492 za serikali.
Pia toka miaka 4 ipite shule hijawahi kutoa daraja la kwanza. kwa pamoja wazazi na walimu walikubaliana kuhakikisha mwaka huu wanapata dara la kwanza kwa vijana wengi. nao wanafunzi walimuahidi mkuu wa wilaya kujituma katika ili waweze kufaulu.
Katika taarifa yake Mkuu wa shule Mwalimu Magayo ambae amehamia miezi 3 iliyopita kutoka shule ya sekondari Lugalo alimwambia Mkuu wa wilaya kuwa kumeibuka changamoto ya vijana kuvuta bangi kwenye korongo la jirani jambo ambalo linahatarisha afya na tabia za vijana.
Mh Kasesela alimtaka Kamanada wa polisi kuwasaka wauzaji na wavutaji bangi harakasana na apewe taarifa ndani ya siku 7 wakiwa wako ndani. Pia aliwaasa wazazi kutoa taarifa wanapo waona wavuta bangi na wauzaji kwney maeneo yao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni