.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 6 Mei 2016

MTUHUMIWA WA KWANZA WA MASHAMBULIZI YA NGONO JIJINI COLOGNE APANDISHWA KIZIMBANI

Kesi ya kwanza ya makosa ya ngono inaendelea Jijini Cologne nchini Ujerumani kuhusiana na tuhuma za mashambulizi ya udhalilishaji wa kingono kwa wanawake usiku wa mwaka mpya.

Kesi hiyo inamhusu kijina wa Algeria mwenye umri wa miaka 26 anayeshtakiwa mahakamani kwa kujaribu kushambulia kingono na wizi.

Raia huyo wa Algeria anatuhumiwa kuwa ni mmoja wa wanaume 10 waliowazingira wanawake kwenye stesheni kuu ya reli Jijini Cologne na kuwafanyia udhalilishaji wa kingono na kuiba.

Jumla ya matukio 1,000 ya makosa ya mashambulizi ya ngono, wizi na udhalilishaji kijinsi yaliripotiwa kufanywa na raia wa kigeni wa Kaskazini mwa Afrika na Waarabu nchini Ujerumani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni