Mwili wa Mama Lucy Kibaki, ambaye ni
mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki umewasili leo Jijini
Nairobi nchini Kenya ukitokea Uingereza.
Mwili wa Mama Kibaki, umekuja na
ndege ya Shirika la Ndege la Kenya KQ, iliyowasili kwenye uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta majira ya saa kumi na moja
alfajiri.
Katika ndege hiyo pia alikuwemo rais
mstaafu Mwai Kibaki na familia yake na marafiki waliokuwa na Mama
Kibaki London kwa matibabu na kufariki.
Rais Uhuru Kenyatta na mkewe
Margaret walikuwepo uwanja wa ndege kuupokea mwili wa Mama Lucy
Kibaki.
Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki akishuka kwenye ndege iliyobeba mwili wa mkewe
Rais Uhuru Kenyatta akimpa mkono wa pole rais mstaafu Mwai Kibaki mara tu baada ya kuwasili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni