Ndege ya shirika la ndege la
EgyptAir iliyoripotiwa kupotea angani kati ya Paris na Cairo,
imeanguka rais wa Ufaransa Fancois Hollande amethibitisha.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320
imetoweka mashariki mwa Mediterranean, ikiwa na abiria 56 wakiwemo
watoto watatu, watumishi saba wa ndege pamoja na maafisa usalama
watatu.
Abiria wa ndege hiyo walikuwa
Wamisri 30, Wafaransa 15, Muingereza mmoja Wairaki wawili na watu
kutoka mataifa ya Canada, Ubelgiji, Kuwait, Saudi Arabia, Algeria,
Sudan, Chad na Ureno.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni