KIUNGO wa Mbeya city fc , Ramadhani Chombo ‘Rendondo’ ameionya
timu ya Yanga ya jijini Dar Es Salaam kuwa ijiandae vya kutosha
itakapokuja jijini hapa mwanzoni mwa juma lijalo kwa ajili ya mchezo wa
ligi kuu ya soka Tanzania bara kati ya timu hizo mbili uliopangwa
kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mei 10 mwaka huu.
Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo, Redondo aliyekosa michezo
miwili ya awali kupisha majeraha ya mguu kabla ya kurejea na kuichezea
City kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar aliweka wazi kuwa ana imani
kubwa na kikosi cha sasa cha timu yake, hasa baada ya ujio kocha Kinnah
Phiri aliyefanikiwa kuyaondosha ‘makandokando’ yote yaliyokuwa
nasababisha timu kufanya vibaya kwenye michezo iliyopita.
Nadhani Yanga wanatakiwa wajiandae vizuri, wanakuja
kukutana na kikosi cha City ambacho kiko kwenye wakati mzuri hivi
sasa,hivyo wasitegemee mteremko,ujio wa kocha Phiri umeiimarisha zaidi
timu yetu, ametupa muongozo mzuri na amefanya kazi kubwa kuweka timu
sawa, hivyo hao wanaokuja wajue watakutana na upinzani mkali,timu yetu
sasa inacheza tofauti sana na ilivyokuwa inacheza hapo mwanzo, alisema.
Akiendelea zaidi Redondo, aliyewahi kucheza kwa mafaniko kwenye
timu za Ashanti, Simba na Azam Fc alisema kuwa anafahamu mchezo huu
utakuwa mgumu pande zote kwa sababu kila timu inahitaji matokeo
kulingana na hali ilivyo kwenye msimamo, Yanga ikitaka kujihakikishia
ubingwa na City ikihitaji kujiweaka kwenye mazingira mazuri zaidi licha
ya kuwepo kwa uhakika kuwa itasalia kwenye ligi .
Kuhusu majaaliwa yake kwenye kikosi cha City Redondo alisema kuwa
anaimani kubwa atakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao, na kuweka wazi
furaha yake ya kuwa mchezaji wa timu hii tangu alipojounga nayo mapema
mwezi Januari.
“Nilijiunga na City mapema mwezi januari, nakumbuka
ilikuwa ni wakati wa usajiri wa dirisha dogo, binafsi nina furaha
hapa na nitaka kufanya kazi zaidi na kwa uwezo wangu wote kwa sababu
lengo langu ni kuendelea kuwepo, kwa ngumi mimi hii ni timu nzuri
kuliko zote nilizowahi kucheza, kuna wakati najiuliza kwa nini sikuwa
huku mapema lakini hii ni soka na maisha ya mchezo huu ndiyo yalivyo”
alimaliza
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni