.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 5 Mei 2016

TAJIRI WA LEICESTER CITY KUWANUNULIA MERCEDES WACHEZAJI WOTE 30

Mfanyabiashara mkarimu wa Thailand, Vichai Srivaddhanaprabha, mmiliki wa Timu ya Leicester City ameahidi kuwazawadia wachezaji 30 wa timu yake gari kila mmoja, kwa kutwaa ubingwa wa Uingereza.

Imebainika kuwa kila mchezaji atapaga gari aina ya Mercedes B-Class Electric Drive, ambalo linauzwa kwa kiasi cha paundi 32,670, hivyo tajiri Srivaddhanaprabha atatumia paundi milioni moja kwa magari yote.

Bilionea huyo tayari ameiahidi timu hiyo inayonolewa na kocha, Claudio Ranieri, kuwapatia ofa ya kutembelea Jijini Las Vegas Marekani ambapo atagharamia kila kitu, kutokana na mafanikio waliyoyapata.
       Gari aina ya Mercedes B-Class Electric Drive watakalo nunuliwa wachezaji
                           Tajiri mmiliki wa Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni