.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 17 Mei 2016

WAFANYABIASHARA WA MADINI WALALAMIKIA KUDHALILISHWA

                                                                                              Na Woinde Shizza ,Arusha

Chama cha wanunuzi na wauzaji wa Madini Tanzania TAMIDA kimetoa tamko la kulaani kitendo cha uongozi wa Halmashauri ya Simanjiro kuwavamia wafanyabiashara wa madini wa jijini Arusha maofisini wakiwa wameambatana na Askari wenye silaha za moto na pingu kuwalazimisha kulipa kodi ya tozo ya huduma ya Madini.

Akitoa tamko hilo katika mkutano wa wafanya biashara wa Madini uliofanyika katika Ofisi za wizara ya madini Kanda ya Kaskazini jijini hapa Makamu mwenyekiti wa TAMIDA Thomas Munis alisema kitendo hicho hakikubaliki na kimelenga kuwadhalisha wafanyabiashara hao pamoja na wateja wao.

Thomas aliutaka uongozi wa Wilaya ya Simanjiro kukaa chini na kukubaliana namna ya ulipaji wa tozo hiyo inayofikia kiasi cha shilingi Milioni 20 hadi 60 kwa mwaka, jambo ambalo alisema hawawezi kulipa mara mbili kwa halimashauri ya Arusha pamoja na Halimashauri ya Simanjioro.

"Sisi kama wafanyabiashara hatupingi kulipa kodi yoyote ya madini ili tunacho sikitishwa nacho ni hatua ya uongozi wa Simanjiro kutufuata maofisini wakiwa na silaha za moto na pingu, kutaka tulipe kodi Huduma ambayo kimsingi tumekuwa tukilipa kila mwaka katika halimashauri ya Arusha", Alisema Thomas.

Aidha aliongozea kusema kuwa wao kama wafanyabiashara wa madini hawapingi kulipa kodi yoyote inayotozwa kutokana na biashara ya madini ila wanachopinga kodi hiyo kutozwa mara mbili kwa mwaka katika halimashauri zote swala ambalo wameliomba serekli kupitia wizara ya madini kuingilia kati swala hilo na kutatua mkanganyiko huo.

Wakati huo afisa madini kutoka ofisi hiyo ya kanda Bwana Erick Mpesa amesema kuwa wao kama kama wasimamizi wa madini katika kanda hii wana ngoja mafikiano ya pande zote mbili ikiwemo halimashauri ya Simanjiro pamoja na jiji la Arusha juu ya Tozo hiyo ya huduma ya Madini.

Kwa upande mwanasheria Jiji la Arusha Bahati chojo amesema kuwa sheria inaelekeza wazi kuwa kampuni yoyote inayofanya bishara ya madini inapaswa kulipa tozo ya huduma kule ilipo ikiwemo kulipa kule ilipo ofisi pamoja na maeneo ya matawi ya ofisi hizo.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni