.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 17 Mei 2016

UTATA KABURI LA SHEIKH ROBERT KUSHUGHULIKIWA HARAKA

Shaka akiwa na ujumbe wake waliozuru katika kaburi la mwandishi gwiji wa
vitabu vya fasihi andishi na simulizi marehemu Shaaban Robert kijiji cha Mjimwema mkoani Tanga

Na Woinde Shizza,Tanga

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM) umesema utaieleza serikali mkoani Tanga kuondosha utata na mivutano iliopo katika kijiji cha Mjimwema kati ya familia mbili husika mahali ambako amezikwa mwandishi
bingwa wa vitabu vya fasihi simulizi na uandishi Marehemu Shaaban
Robert.

Tamko hilo limetamkwa na Kaimu katibu Mkuu wa Uvccm Shaka Hamdu Shaka aliyefika katika kaburi la Mwandishi huyo nguli katika Afrika mashariki aliyezaliwa January 1, 1909 na kufariki Juni 20, 1962 .

Shaka mara baada ya kusafisha kaburi la marehemu na kuomba duwa akiwa na ujumbe wake alielezwa na mjukuu wa marehemu Khatib Mwinjovu kwamba
mahali hapo alipozikwa babu yake Shaaban Robert pamekuwa na mivutano isio na ulazima toka upande wa familia ya mke wa marehemu Robert.

Alisema kaburi hilo ni alama kuu katika Taifa letu hivyo halipaswi
kuandamwa kwa mivutano au misuguano isio na sababu na kuahidi kwamba
seeikali itatumia uwezo wake kuleta mapatano haraka.

"Nitaongea haraka na mkuu wa mkoa wa Tanga kuhusu utata huu. UVCCM ingependa kuona kaburi la mwandishi huyo bingwa anayetajika duniani
linatunzwa kwa heshima zote. Huyu mtu ametumia maisha yake yote kuandika ili kuvielimisha vizazi na vizazi hadi sasa.

Aidha shaka aliitaka jamii kutambua na kuheshimu nguvu alizozitumia
marehemu Shaaban Robert katika uhai wake ambazo sasa alisema zinafaa katika kizazi hiki hadi kingine wakati yeye akiwa hapati tija wala faida.

Kwa upande wake katibu wa ccm mkoa wa Tanga Shija Othman Shija alisema
uamuzi wa UVVCM kuja kulizuru kaburi hilo ni tendo la kiungwana hivyo
akatoa wito kwa jumuiya nyingine nazo kuiga mfano huo.

Shija alisema ni jambo lisilowezekana kuzungumzia nchi yetu kabla na
hata baada ya uhuru bila kulitaja jina la marehemu Shaaban Robert
kutokana na mchango wake mkubwa hasa katika mitaala ya elimu na ukuzaji
lugha ya kiswahili.

"Shaaban Robert amekuwa nguzo na kioo ambacho hakutavunjika wala kuingia nyufa wakati wote, maandiko yake yatabaki katika kurasa muhimu toka kizazi kimoja hadi kingine "alisems katibu huyo wa ccm mkoa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni