Mchezaji wa Argentina Angel di Maria
amesherehekea goli alilofunga katika ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya
Chile, kwa kuomboleza kifo cha Bibi yake aliyefariki dunia kabla ya
kuanza michuano ya Copa America.
Katika mchezo huyo ambao Argentina
walifanikiwa kulipa kisasi cha kufungwa na Chile, Angel di Maria na
Ever Banega waliweza kuitakatisha timu yao ya taifa kwa kufumania
nyavu huku Lionel Messi akiwa benchi kutokana na maumivu ya mgongo.
Angel di Maria akicheza muziki na marehemu Bibi yake wakati wa uhai wake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni