Bondia Lennox Lewis atakuwa ni
miongoni mwa watakaobeba jeneza lenye mwili wa Muhammad Ali siku ya
mazishi yake Ijumaa hii katika mji wa Louisville, Marekani.
Bondia huyo maarufu Uingereza
atakuwa na muigizaji filamu, Will Smith, ambaye aliigiza kama Ali
kwenye filamu akisaidiana na familia pamoja na marafiki kubeba jeneza
la Muhammed Ali.
Lewis, ambaye bado ni bingwa
asiyepingika wa uzito wa juu, amekuwa mtu wa karibu na Ali kwa miaka
mingi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni