.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 15 Juni 2016

ASPER MAKALA WA MCDI KILWA ATWAA TUZO NYINGINE HUKO USA

Picha Hivi karibuni Jasper Makala Akikabidhi Tuzo ya Whitley Award Kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi. Na Abdulaziz Video,Lindi
Mkurugenzi wa MCDI,Jasper Makala (Kulia) Akipokea Tuzo ya Mwaka 2016 Utunzaji na Uhifadhi wa Misitu toka kwa Dr Gary Knel.Afisa Mtendaji Mkuu Geographic Society jana huko USA.

 
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhifadhi mpingo na maendeleo(MCDI) Mr Makala Jasper Usiku wa  jana huko Washington DC-USA  Ameibuka Kidedea baada ya kushinda Tuzo ya mwaka 2016 iitwayo National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation, Tuzo hiyo ina thamani ya Dolla 25,000.

Jasper Makala Mkurugenzi wa MCDI Yenye makao makuu yake Kilwa Masoko Mkoani Lindi ameiwakilisha vyema Africa na Tanzania Ambapo kwa Kushinda Tuzo hiyo.

Ushindi huo ni Baada ya Kuwashinda Wasiriki wengine 30 Toka bara la Africa na Wenye Uwezo mkubwa na kufanya mchuano kuwa mkali sana.

Iikumbukwe hii ni tuzo ya pili ndani ya miezi miwili ambapo Makala Jasper  aliwania tuzo za Whitley huko nchini Uingereza ambapo pia alishinda tuzo hiyo ambayo ilikuwa na thamani ya Paundi  £35, 000.Zaidi ya Milioni 100 za Kitanzania

Ushindi huo unatokana na Mawasilisho ya Utunzaji Shirikishi na Uhifadhi wa Misitu

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni