Timu ya Cleveland Cavaliers
imeshinda ubingwa wa NBA kwa kuwashinda mabingwa watetezi Golden
State Warriors kwa pointi 93-89 katika fainali ya 7 iliyopigwa
jumapili.
Ushindi huo ni wa kwanza mkubwa
kuwahi kupata kwa timu ya Cleveland Cavaliers tangu mwaka 1964.
Mchezaji LeBron James alikuwa ni
chachu ya ushindi na kutangazwa Mchezaji Ghali Kuliko Wote (MVP) kwa
mwaka huu, ambapo alifunga pointi 27, rebaundi 11 na kutoa msaada
mara 11.
Lebron James akitokwa machozi kwa furaha huku akikumbatia kombe la NBA
LeBron James akiwa na watoto wake akiongea na waandishi wa habari baada ya ushindi
Kilio cha ushindi: Lebron James akimkumbatia mchezaji mwenzake huku akiangua kilio baada ya kupata ushindi




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni