Cristiano Ronaldo amekosa penati
kwenye kipindi cha pili katika mchezo ambao umewachanganya mno Ureno
na kapteni wao, ulioishia kwa sare ya 0-0 Jijini Paris dhidi ya
Austria.
Katika mchezo huo Ronaldo alipiga
mpira wa adhabu uliogonga mwamba, baada ya beki wa Austria Martin
Hinteregger kumpiga mweleka chini, na kisha baadaye kupachika goli la
kichwa ambalo lililakaliwa kutokana na kuwa ameotea.
Hata hivyo sifa zote zinabaki kwa
golikipa wa Austria Robert Almer, ambaye alifanya kazi nzuri kwa
kuokoa kwa umahiri mkubwa michomo ya wachezaji wa Ureno kama ya Luis
Nani pamoja na Cristiano Ronaldo.
Cristiano Ronaldo akipiga penati ambayo alikosa kufunga goli
Cristiano Ronaldo akiwa juu angani kupiga mpira wa kichwa
MISMAMO WA KUNDI F




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni