Goli la kujifunga la dakika za
mwisho la Birkir Saevarsson limeinyima Iceland ushindi muhimu na
kutoa fursa kwa Hungari kuelekea kutinga hatua ya 16 bora katika
michuano ya Euro 2016 inayofanyika nchini Ufaransa.
Katika mchezo huo Gyfli Sigurdsson
aliipatia Iceland goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza baada ya
kufanikiwa kutikisa nyavu kwa mkwaju wa penati waliozawadiwa baada
kuchezewa rafu ndani ya eneo la penati.
Katika mchezo huo Hangari walitawala
mno na kumiliki mpira lakini hata hivyo walichanganywa na ukuta imara
wa timu ya Iceland. Jitihada zao zilizaa matunda pale krosi ya
Nemanja Nikolic ilipotumbukizwa kimiani na Saevarsson na matokeo kuwa
1-1.
Gyfli Sigurdsson akiachia shuti la mkwaju wa penati
Mpira wa penati uliopigwa na Gyfli Sigurdsson, ukijaa wavuni na kumuacha kipa wa Hangari hoi baada ya kupotea mahesabu
Birkir Saevarsson akijifunga goli katika harakati za kuokoa krosi ya Nemanja Nikolic



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni