Lionel Messi amefika rekodi ya
Gabriel Batistuta yakuifungia Argentina magoli 54, wakati timu hiyo
ya taifa ikiifunga Venezuela kwa magoli 4-1 na kutinga nusu fainali
ya michuano ya Copa America.
Katika mchezo huo mshambuliaji huyo
wa klabu ya Barcelona mbali na kufunga pia aliwatengenezea magoli
Gonzalo Higuain aliyefunga magoli mawili na Erik Lamela na kuisaidia
Argentina kutinga hatua ya nusu fainali ambapo watakutana na wenyeji
Marekani.
Gonzalo Higuain akimyanyua juu Lionel Messi baada ya kumpatia pande la kufunga goli


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni