Mshambuliaji Cristiano Ronaldo
amefunga magoli mawili wakati Ureno ikiwa na wachezaji 10,
ikiifurumushia Estonia mvua ya magoli 7-0, katika mchezo wa wa mwisho
wa kujiandaa na michuano ya Euro 2016.
Katika mchezo huo Ricardo Quaresma
naye alitigisa nyavu mara mbili, na Danilo, Eder moja kila mmmoja
huku Karol Mets akikamilisha kichapo hicho kwa kujifunga.
Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa
Ronaldo kushuka dimbani tangu ashinde Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya
mwezi uliopita akiwa na timu yake ya Real Madrid.
Cristiano Ronaldo akiruka kuupiga mpira kwa kichwa kilichozaa goli
Ricardo Quaresma akiachia shuti kati kati ya mabeki wa Estonia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni