Timu ya Taifa ya Brazil imeichakaza
Haiti kwa magoli 7-1, wakati Philippe Coutinho akifunga magoli matatu
yaani hat-trick katika mchezo wa michuano ya Copa Amerika.
Katika mchezo huo Philippe Coutinho
alikuwa wakwanza kuzifumania nyavu, ambapo pia Renato Augusto
naye aliifungia Brazil magoli mawili wakati kikosi cha Dunga
kikifanya mauaji makubwa.
Mchezaji aliyetokea benchi Gabriel
Barbosa na Lucas Lima wote nao waliifungia Brazil na kuifanya Brazil
kujikusanyia pointi nne, huku ikiwa na mchezo mmoja wa mwisho katika
kundi lao dhidi ya Peru.
Philippe Coutinho akiachia shuti lililojaa wavuni
Renato Augusto akiangalia mpira wa kichwa alioupiga ukijaa wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni