Wapalestina wawili wenye bunduki
wameuwa watu wanne na kujeruhi sita baada ya kufyatua risasi kwenye
eneo la wazi la manunuzi na hoteli kati kati ya Jijini Tel Aviv,
Mamlaka za Israeli zimesema.
Mashambulizi hayo yamefanyika kwenye
maeneo mawili tofauti katika Soko la Sarona, lililopo karibu na
Wizara ya Ulinzi ya Israel na Makao Makuu ya jeshi.
Polisi wamesema watu hao wawili
wenye silaha wanatokea Yatta, katika kijiji cha Palestina kilichopo
karibu na mji wa Hebron huko West Bank.
Polisi wa Israeli wakimdhibiti mtu mmoja na kumvua nguo baada ya kumshuku kuwa huenda alikuwa amevaa milipuko
Madaktari wakihaha kujaribu kuokoa maisha ya mtu mmoja aliyejeruhiwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni