.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 16 Juni 2016

IRINGA WATAKIWA KUJIKITA KATIKA KILIMO CHA VIAZI VITAMU

Meneja Mkuu kiwanda cha Tosti ambao ndio wanunuzi wakubwa wa viazi akitoa melezo. Kiwanda hiki kipo Iringa na kina mahitaji ya viazi kiasi cha tani 150 kwa wiki za viazi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya Iringa Mh Richard Kaseselaakionyesha moja ya viazi vitamu.
Meneja mradi wa VISTA Fred Grant akiongea kumkaribisha Mgeni Rasmi Mh Richard Kasesela
Sheikh Mwang'amilo akimpongeza Mkuu wa Wilaya na kuwaomba wananchi walime viazi vitamu kwa wingi na kuacha kunywa ovyo pombe.

Mh Kasesela akifurahia Juice ya Viazi Vitamu na watoto Fabiana na Telephina wa Kijiji cha Luganga 


Alitoa rai hiyo katika siku ya Wakulima katika kijiji cha Luganga kata ya Ilolo Mpya tarafa ya Pawaga. Hafra hiyo iliyo andaliwa na mradi wa Viazi Lishe "Viable Sweet Potato Technlogies in Africa-VISTA na kufadhiriwa na seriakli ya watu wa Marekani (USAID) unajumuisha Halmashauri 7 ikiwemo IRinga, Wangingombe, Gairo, Mufindi, Ulanga,Mbozi na Chunya. 

Katika mradi huo wakulima wanahamasishwa kulima viazi lishe kwa ajili ya afya ya mama na mtoto na pia kwa ajili ya biashara ambapo bidhaa kama juice, chapati, kakau(clips), tambi, mkate , maandazi na bidhaa zingine nyingi huweza kutengenezwa ili kukuza kipato. 

Akimkaribisha mgeni rasmi Meneja wa Mradi wa VISTA Bwana Fred Grant alisema mradi huu uko katika mwaka wa 2 na ni wa miaka 3 ni muhimu Tanzania ikaanza kufikiria jinsi ya kuuendeleza nchi nzima kwani manufaa yake ni makubwa. 

Sherehe hizo pia zilihidhuriwa na waakilishi kutoka Halmashauri zote 7 zinazonufaika na mradi huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni