Timu ya taifa ya Italia imecheza kwa
ufundi zaidi huku ikitandaza kandanda safi na kufanikiwa kuwaondoa
mabingwa watetezi kombe la Euro 2016 timu ya taifa ya Hispania kwa
magoli mawili kwa bila.
Katika mchezo huo beki mkongwe
Giorgio Chiellini alifunga goli la kwanza akitumbukiza mpira wa
karibu na lango baada ya David de Gea kuupangua mpira wa adhabu
uliopigwa na Eder katika kipindi cha kwanza.
Mchezaji wa klabu ya Southampton
Graziano Pelle alikamilisha ushindi kwa kufunga goli katika dakika
majeruhi kwa umbali wa yadi nane.
Beki mkongwe
Giorgio Chiellini akifunga goli la kwanza
Graziano Pelle akifunga goli la pili kwa Italia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni