Orodha ya wachezaji ambao walikuwa kwenye kikosi cha Mbeya City fc
msimu uliopita na mikataba yao kufikia tamati baada ya kumalizika kwa
ligi kuu ya vodacom Tanzania bara mei 22 tayari imetolewa
ikiwataja nyota saba kutokuwepo tena kikosini msimu ujao.
Muda mfupi uliopita, Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe amesema kuwa,
wachezaji saba wanaotajwa kwenye orodha hii ni wazi mikataba yao
imemalizika na klabu haitafanya tena mazungumzo yoyote na tayari
wamesha taarifiwa juu ya hilo.
“Mikataba yao imemalizika, tumekwisha wataarifu kuwa
hatutakuwa na mazungumzo mapya, hili soka kutoka timu moja kwenda
nyingine ni jambo la kawaida hivyo tunawatakia kila la heri kwenye
maisha mapya ya soka watakayo kutana nayo” alisema.
Kwenye orodha hiyo yupo mlinda mlango Haningtony
Kalyesubula, walinzi ni Yusuph Abdalah Sisalo,Deo Julius,Hamad
Kibopile,Yohana Morris, Richard Peter Chundu na mshambualiaji Temmi
Felix.
Katika hatua nyingine Kimbe amesema kuwa klabu bado inafanya
mazungumzo na baadhi ya nyota ambao mikataba yao imemalizika lakini
bado wanayo nafasi ya kuendelea kukitumikia kikosi cha City kwa mujibu
wa mapendekezo ya kocha Kinnah Phiri, huku pia mazungumzo ya wachezaji
wengine ambao bado wana mikataba lakini hawapati nafasi ya kucheza
yakiendelea ili kuona ni jinsi gani wanaweza kupata nafasi ya kuendeleza
vipaji vyao.
Orodha ya wachezaji hao pamoja na wale wanaoendelea kuitumikia klabu itatolewa hapo baadae.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni