Mshambuliaji
Daniel Sturridge ameifungia Uingereza goli katika dakika za majeruhi
na kuisaidia kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wales na
kupata ushindi wa kwanza katika michuano ya Euro 2016.
Kipa
wa Uingereza Joe Hart alifanya kosa la kizembe na kuruhusu goli la
mpira wa adhabu uliopigwa na Gareth Bale kutoka umbali wa yadi 30,
kuifanya Wales kuongoza katika kipindi cha kwanza huko Lens,
Ufaransa.
Kufuatia
hali hiyo Roy Hodgson ambaye ni kama alikuwa amekalia kuti kavu
alifanya mabadiliko na kuwaingiza Jamie Vardy na Daniel Sturridge waliofunga goli kila mmoja na
kuwatoa Raheem Sterling na Harry Kane.
Daniel Sturridge akifunga goli la pili la Uingereza katika dakika za majeruhi
Gareth Bale akipiga mpira wa adhabu uliojaa wavuni na kuandika goli la kwanza la Wales



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni