Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akiwaongoza Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo kumpa pole Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) kwa kufiwa na mdogo wake, Fredina Mbasha. Wakuu hao wa Idara walienda kumfariji kiongozi huyo nyumbani kwa marehemu, Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akimfafannulia jambo Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa
Wizara hiyo, Haji Janabi (kulia) wakati Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo
walipoenda kumfariji kiongozi huyo, baada ya kufiwa na mdogo wake, Yombo
Machimbo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Nonela Sisamo, Shemeji wa
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edwin Makene (kulia) akimpa pole Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira kwa kufiwa na mdogo wake, Fredina Mbasha. Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo walienda kumfariji kiongozi huyo nyumbani kwa marehemu, Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jenita Ndone akimpa pole Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) kwa kufiwa na mdogo wake, Fredina Mbasha. Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo walienda kumfariji kiongozi huyo nyumbani kwa marehemu, Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni