.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 7 Juni 2016

VIONGOZI WA DINI HUBIRINI AMANI KATIKA MATHEHEBU YENU :MKUMBO

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Charles mkumbo akiwa anaongea na viongozi wa dini zote wa mkoa wa Arusha hii ikiwa ni mkutano wa kwanza wa kufanya na viongozi wao tangu kuwasili mkoani hapa
Picha ya juu na chini ikionyesha baadhi ya mashehe ,askofu,wachungaji ,madiwani pamoja na maaskari waliothuria katika mkutano ulioandaliwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuongea na viongozi wa dini juu ya namna gani ya kuendelea kudumisha amani ya nchi na mkoa kwa ujumla mkutano uliofanyika katika ukumbi wa polisi mesi uliopo jijini hapa

Mashehe kutoka katika misikiti mbalimbali ya mikoa wa Arusha wakiwa ktika picha ya pamoja na kamanda wa polisi pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha akiwemo meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro
Wachungaji kutoka katika mazehebu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha pamoja na meya wa jiji
Pia kamanda wa polisi mkoa wa Arusha aliwataka baadhi ya waandishi wa habari waliouthuria katika mkutano huo kupiga na viongozi hao picha ya pamoja hapa waliosimama nyuma wote ni waandishi wa habari waliouthuria siku hiyo.
 
 Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Charles mkumbo amewataka
viongozi wa dini mkoani Arusha kuakikisha wanaubiri amani katika
nyumba zao za ibada ili kuweza kuweka hali ya usalama na amani katika
mkoa wa Arusha.

Aliyasema hayo juzi katika kongamano la siku moja la viongozi wa
dini mkoani Arusha katika kongamano la viongozi wa dini mkoa Arusha
lilondaliwa na kamanda mkumbo na kuwashirikisha madiwani wa jiji la
Arusha pamoja na viongozi wa kisiasa .

Aidha kwa upande wake meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro akiwa kama
mmojawapo wa washiriki wa kongamano hilo na kueleza kuwa ujio
kongamano hilo liloandaliwa na kamanda Mkumbo ni kuonyesha mwelekeo
mzuri wa kulinda amani ya Arusha.
 
Aidha pia meya wa jiji la arusha alitumia muda huo kuwaasa
wafanyabiashara hususa ni wauzaji wa chakula pamoja na vinywaji vikali
kuhakikisha wanafanya biashara zao kwa kufuata sheria ambapo alisema
kuwa airuhusiwi sehemu ambayo inauza chakula kuuza vinjwaji vikali
ikiwemo bia pamoja na pombe
 
"unaja sasa ivi tunataka tufanya mji wetu safa hairusiwi mtu anaeuza
pombe kuuza chakula na chakula kuuza pombe pia kumekuwa na tatizo la
sehemu nyingi apa mjini kufungua mziki kama wanavyotaka sasa sasa hivi
airuhusiwi mtu yeyote kufungua mziki mkubwa iwe kwenye bar au grosary
pasipo kuwa na kibali rasmi kutoka sehemu husika hii pia inawahusu
hawa vijana ambao unakuta wanaingiza nyimbo kwenye cd yaani unakuta
kafungua mziki hadi kero inakuwa usumbufu sasa kuanzia sasa hivi
airusiwi mtu kufungua mziki mkubwa pasipo kibali"alisema Kalist
Aidha alisema anaimani swala hili litafanikiwa kwakuwa polisi
wameshaamua kushirikiana nao na watafanya kazi kwa umoja hadi
waakikishe mji wao unakuwa tulivu na msafiki .

Wakati huo huo mchungaji wa kanisa la Angilkana mchungaji Kenoni
Kajembe alisema kuwa wao kama viongozi wa dini mkoani hapa wana
jukumu kubwa la kuakisha kwamba dhima ya amani inajulikana kwa waumini
wao wanaowaongoza.

Kongamano kama hilo linatarajiwa kufanyika mfululizo katika wilaya
sita zilizobakia za mkoa wa Arusha na wiki hii na na pia kamanda
Mkumbo anatarajiwa kufanya kongamano la amani kama hili na viongozi wa
serekali za mitaa ndani ya jiji la Arusha.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni