.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 7 Juni 2016

SEREKALI YATAKIWA KUANGALIA KWA MAKINI BAJETI YAO YA MWAKA WA FEDHA 2016/2017 KWA KUANGALIA ZAIDI SEKTA YA AFYA PAMOJA NA ELIMU

Na Woinde Shizza,Arusha

BAADHI ya wananchi wa mkoani Arusha wameiomba serikali kuhakikisha
bajeti ijayo ya mwaka wa fedha inawaangalia kwa jicho la pili wananchi wenye kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kukidhi baadhi ya mahitaji yao kwa kupunguza bei ya bidhaa ili kupunguza makali ya maisha

Serikali ya awamu ya tano kama itaweza kupunguza baadhi ya kodi katika mahitaji muhimu basi maisha ya wananchi wenye kipato cha chini yataweza kuboreka na hivyo umaskini utapungua kwa kiwango kikubwa tofauti na sasa.
 

Hayo yameelezwa na wananchi wa jiji la Arusha wakati wakiongea na
na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na bajeti ijayo ya serikali ambapo wamedai bajeti hiyo inatakiwa kulenga kwenye vipaumbele maalumu ambavyo
vinagusa maisha ya wananchi ya kila siku na sio ya kulenga watu wenye
vipato vya juu tu.


Kwa upande wake mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina La Enjo John alisema kuwa kwa sasa maisha ya watanzania hususani wenye kipato cha chini wanashindwa kumudu milo mitatu kwa siku kutokana na baadhi ya bidhaa kuuzwa kwa bei ya juu sana kitu ambacho kinachangia kuongeza kiwango cha umaskini na lishe duni kwenye baadhi ya familia.

Alitolea mfano wa bidhaa za sukari, mchele, mafuta, nguo ambapo kutokana na kipato ambacho wanapata baadhi ya watanzania kinasababisha wakose mahitaji hayo ambayo ni muhimu kwa siku.
 

“bajeti hiyo inatakiwa itoe vipaumbele kwenye chakula kodi zisizo na maana ziondolewe kabisa chakula kiwe na uhakika na kama itakuwa hivyo watu wengi watapata fursa ya kuwa na afya njema na kisha kulitumika taifa letu” aliongeza Emanulel Peter

Aliongeza kuwa bajeti ya serikali inatakiwa kutoa vipaumbele kwenye sekta ya elimu,afya,pamoja na uwekezaji wa ndani.

Alisema Kwa upande wa sekta ya afya kunatakiwa kuwe na huduma bora
ambapo huduma hizo ni pamoja na wingi wa vituo vya afya, lakini pia hata dawa ,nyumba za watumishi, pamoja na huduma ya mama na mtoto kwa kuwa kwa maeneo ya vijijini wanawake wengi wanafariki wakati wakiwa wanajifungua.


Kwa upande wa wanawake wa jiji la Arusha walisema kuwa bajeti inatakiwa ikidhi mahitaji muhimu hususani ya elimu kwani asilimia kubwa ya wanawake wanabeba majukumu ya kusomesha familia zao.

Mmoja wa wanawake hao,ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Nasholi
Aggness Limo alisema kuwa bajeti inayokuja ilenge kuboresha mazingira ya walimu ikiwepo nyumba za kuishi ,kuboreshewa maslahi pamoja na wanafunzi kuongezewa vitabu vya kiada na ziada kwani vimekuwa ni changamoto kubwa sana mashuleni.
 

Nae mmoja wa askari usalama alisema kuwa ni vema bajeti inayokuja ikatoa vipaumbele kwa maaskari kuboroshewa mishahara ,kuongezewa vitendea kazi vya kisasa na kujengewa nyumba za kuishi kwani baadhi ya maaskari wanaishi nyumba ambazo hazina hadhi na wao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni