Kocha machachari Jose Mourinho
amekubali yaishe baada ya kuona huenda atashindwa na Daktari mwanamke
Eva Carneiro katika kashfa inayomkabili iliyofikishwa mahakamani.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na
sasa Manchester United ameamua kuzizima tuhuma za udhalilishaji wa
kijinsia, kabla ya Dk. Eva Carneiro kuweka wazi mbele ya umma tuhuma
hizo mahakamani.
Mourinho na klabu ya Chelsea
wamekubali kumlipa Dk. Carneiro paundi milioni 5, ambaye anadai kuwa
kocha huyo alimuita 'Binti wa kahaba'.
Mourinho anadaiwa kutoa kauli hiyo
baada ya kuchukizwa Dk. Carneiro kwa kuwa na papara ya kukimbia
dimbani kuwahi kumtibu mchezaji katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Uingereza.
Daktari Eva Carneiro
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni