.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 8 Juni 2016

PICHA ZA MATUKIO YA UZINDUZI WA MPANGO WA PILI WA MAENDELEO WA TAIFA WA MIAKA MITANO 2016/17/2020/21, DODOMA JUNI 7, 2016

Kikundi cha ngoma cha Nyati cha mkoani Dodoma kikitumbuiza wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 hadi 2020/21, utakao gharimu shilingi Trilioni 107, katika Ukumbi wa Chuo Cha Mipango Dodoma, Juni 7,2016
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka Mitano utakao gharimu shilingi Trilioni 107, huku Mawaziri Prof. Jumanne Maghembe na Prof. Sospter Muhongo nao wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma, Juni 7, 2016
Mbunge wa Mhe. Chalinze Ridwani Kikwete, akicheza ngoma ya kigogo inayochezwa na Kikundi cha ngoma cha Nyati cha mkoani Dodoma, wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 hadi 2020/21, utakao gharimu shilingi Trilioni 107, katika Ukumbi wa Chuo Cha Mipango Dodoma, Juni 7,2016
Mbunge wa Korogwe Vijijini Mhe. Steven Hillary Ngonyani 'Maji Marefu' akicheza ngoma ya kigogo inayochezwa na Kikundi cha ngoma cha Nyati cha mkoani Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 hadi 2020/21, utakao gharimu shilingi Trilioni 107, katika Ukumbi wa Chuo Cha Mipango Dodoma, Juni 7,2016
Mmoja wa wadau wa maendeleo, akionesha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka 5, baada ya kukabidhiwa na Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa, katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma, Juni 7, 2016
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia, akisoma kitabu cha mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano 2016/17/2020/21, utakao gharimu shilingi Trilioni 107, baada ya kuzinduliwa rasmi katika Chuo cha Mipango Dodoma Juni 7, 2016

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni