Afisa Mshauri wa Masuala ya Utawala Bora PS3, Nazar Sola akitoa Elimu kwa Madiwani juu ya Utekelezaji wa Mifumo ya Utendaji na Utoaji Hudu
Madiwani wa Halmashauri za Wilaya ya Kilwa na Ruangwa Mkoani Lindi Zimeanza Utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) kwa Kupatiwa Mafunzo ya Siku 4 na Kuratibiwa na Tamisemi
Kuanza kwa Hatua Hiyo kunafuatia kumalizika kwa Mafunzo kwa Watendaji wa Halmshauri 6 Za Mkoa wa Lindi juu ya Namna ya Kushiriki na Kutekeleza Mradi huo Utakaotekelezwa kwa Kipindi cha Miaka 5 Ijayo
Akifungua Mafunzo hayo,Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi amezitaka Halmashauri Hizo Kufuatilia kwa Umakini Mafunzo yanayotolewa na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo ili Kupata Uelewa Juu ya Uendeshaji wa Halmashauri
‘’ Madiwani ni kiungo muhimu baina ya serikali na watendaji wa serikali madiwani Musipokuwa Vizuri Mtaburuzwa na Watendaji hususan katika Utendaji na Utekelezaji wa Miradi hasa Ikiwa Diwani Una Tabia ya Kuomba omba na Kukopa kwa Mkurugenzi au Mkuu wa Idara Lazima Mjipime Nyie Ndio wamiliki wa Halmashauri au hamjijui?’’Alimalizia Zambi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni