Beki wa zamani wa timu ya taifa ya
Nigeria “Super Eagle” Stephen Okechukwu Keshi ambaye pia aliwahi
kuwa kocha wa timu hiyo ya taifa amefariki dunia.
Keshi (54) amefariki dunia usiku wa
kuamkia leo akiwa Benin, na taarifa za kutokea kifo chake
zomethibitishwa na Ben Olaiya.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano
wa Shirikisho la Soka nchini Nigeria, Ademola Olajire, naye ameeleza
kuwa Keshi amefariki dunia hospitali alipopelekwa kutibiwa miguu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni