Rais Barack Obama hatohudhuria hafla
ya kumbukumbu na dua kwa bondia Muhammed Ali siku ya Ijumaa, Ikulu ya
Marekani imesema.
Ali alifariki dunia Ijumaa akiwa na
umri wa miaka 74 katika hospitali ya Phoenix, Arizona.
Viongozi wa dunia watakuwa miongoni
mwa maelfu ya watu wataohudhuria dua maalum kwa bondia huyo Ijumaa
huko Louisville, Kentucky, ambako ndipo Ali alipozaliwa.
Ikulu ya Marekani imesema rais Obama
na mkewe Michelle watakuwa kwenye mahafali ya binti yao Malia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni