Kutoka kushoto ni Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Development Studies -UDOM, Edson Baradyana, Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa, Mtaalamu wa Upangaji na Usimamizi wa Miradi -PRO UDOM, Radhia Rajabu, Mhitimu wa kidato cha sita, Aisha Msantu wa Asasi ya Vijana wa Umoja Taifa Tanzania (YUNA) katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Ninajisikia kuelimika na kuelewa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu kiasi ya kwamba ninaweza sasa kuwaelimisha marafiki, vijana wenzangu na familia. Elimu hii hapo awali sikuwa nayo , sikuwa naelewa vyema malengo haya. Ukomo wa mpango huu wa dunia ni mwaka 2030 wakati ambapo mimi nitakuwa na umri wa miaka 40. Nataka kuwa sehemu ya mashuhuda wa mafanikio katika utekelezaji wake na ndio maana nataka kutimiza wajibu wangu kwa kupeleka elimu hii kwa wengine.” anasema Jane, mmoja wa washiriki wa semina.
VIJANA 1000 na wanazuoni 200 wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) wamepatiwa mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani kwa nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma.
Kazi ya kufunza malengo hayo ilifanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi ya Umoja wa Mataifa (UN) kuwezesha uelewa kwa tumaini kuwafanya wananchi hasa vijana kutambua wajibu wao katika kutekeleza malengo hayo.
Mafunzo hayo katika Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ni mwendelezo wa mafunzo yaliyozinduliwa Arusha wiki iliyopita na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez.
Mafunzo hayo yalifanywa kwa kundi la vijana 50 kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania ili waende kusambaza uelewa wa malengo hayo kwa vijana wenzao nchini kote.
Inatarajiwa kuwa zaidi ya vijana elfu 20 watakuwa wamepatiwa mafunzo katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Akizungumza katika kampasi ya UDOM Bw. Rodriguez alisema kwamba Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanahitaji ushirikiano wa watu wote ili kuyafanikisha kama ilivyokusudiwa. Malengo ya Maendeleo Endelevu ukomo wake ni mwaka 2030.
Aliwapongeza wanachuo na wanazuoni kwa kujikita kwao kuelewa Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo ndiyo malengo ya dunia ili kuweza kuyasimamia na kuyatekeleza.
Pia alizungumzia umuhimu wa vijana kushiriki katika masuala ya maendeleo hasa kwa kuzingatia kwamba asilimia 60 ya wananchi wa Tanzania ni vijana.
“Mna wajibu mkubwa kwa vijana wenzenu” alisema Bw. Rodriguez na kueleza kwamba amefurahishwa kuona kwamba vijana na wanazuoni 1,200 wameahidi kuwa walimu na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu majumbani kwao, katika taasisi zao na katika jamii inayowazunguka.
Alisema
katika hilo Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kuhakikisha kwamba
wake kwa waume na vijana wanatekeleza wajibu wao kwa kushiriki vyema
katika mipango ya maendeleo yenye kulenga kufanikisha Malengo ya
Maendeleo Endelevu duniani.
Alisema wajibu wa kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani kunategemea watu wote na hasa vijana.
Akipongeza juhudi za kuelimisha za Umoja wa Mataifa, Profesa Flora Fabian kutoka UDOM, alisema chuo hicho kimefurahishwa kuwa moja ya vituo vya kufunza mabalozi vijana wa kusambaza elimu na wajibu katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu.

malengo hayo ya Dunia ni lazima yajulikane kwa kila mmoja; huku
akiwataka wanazuoni kuyazungumza katika kazi zao za kila siku, katika
tafiti na ripoti kama ilivyo kwa wanafunzi ambao wanastahili kupikwa
kuwa katika nafasi ya kuweza kuchambua malengo hayo kwa kuwa na takwimu
na taarifa sahihi.
Alipongeza uamuzi wa utoaji elimu wa Umoja wa Mataifa na kuamini kwamba watasambaza elimu hiyo kwa vyuo vikuu vyote nchini Tanzania.
Septemba 2015, viongozi kutoka nchi 193 duniani walitia saini Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani. Malengo hayo mapya yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15 huku ikiweka pamoja shughuli za maendeleo ya kijamii, kiuchumi yanayojali mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni