Nyani mmoja amesababisha kukosekana
umeme karibu nchi nzima ya Kenya baada ya kuanguka kwenye eneo muhimu la
mitambo ya umeme.
Nyani huyo aliangukia kwenye
transfoma katika bwawa kuu la kuzalisha umeme Kenya la Gitaru siku ya
jumanne, taarifa ya kampuni ya umeme ya KenGen imeeleza.
Kitendo cha nyani huyo kuangukia
transfoma kilisababisha kujizima na umeme wa megawati 180 kukosekana
jambo lililopelekea maeneo mengi ya Kenya kuwa gizani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni