.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 29 Juni 2016

MAHAKAMA KUU JIJINI ARUSHA YATENGUA UBUNGE WA MH. ONESMO OLE NANGOLE, YAAGIZA UCHAGUZI HUO KURUDIWA UPYA

Kesi iliyokuwa ikiunguruma kuanzia Februari 29 ,2016 katika Mahakam Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo.

Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dkt
Kiruswa alifikisha mahakamani shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi
dhidi ya Mbunge wa Longido, Mh.Onesmo Nangole ( Chadema ).

Akisoma hukumu  hiyo,Jaji Mwagesi alisema kuwa mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa  na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.Katika shauri  hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni:

1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole.

2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole

3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura

4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.

5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo

Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa  pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka
mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;"Kutokana na kuzingatia
viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa
sheria,Natamka kwamba;

Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa  kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni