.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 29 Juni 2016

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA KINGA NA TAHADHARI YA MAJANGA YA MOTO, JIJINI DAR ES SALAAM

Kamishna wa Oparesheni, Rogatius Kipali akisisitiza ufanyaji kazi kwa bidii, nidhamu, uadilifu na weledi kwa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi waUumma inayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Godfrey Peter, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuonyesha mwananchi aliyetembelea Banda la Maonyesho la jeshi hilo jinsi ya kutumia mtungi wa kuzimia moto wa awali, katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idd Chanyika (kulia) akitoa maelezo jinsi ya vifaa vya kinga na tahadhari vinavyotumika kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Michael Shija (kushoto), Kamishna wa Oparesheni, Rogatius Kipali (wapili kushoto) na Naibu Kamishna wa Utawala naFedha, Billy Mwakatage walipotembelea banda hilo Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.

Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lililotumika kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto na maokozi lililopo katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni