Fataki
imelipuka mbele ya wasimamizi wa uwanja wakati mashabiki wa Croatia
walipoanza kurusha fataki hizo uwanjani na kuanza kupigana wenyewe
kwa wenyewe katika mchezo ulioishia kwa sare ya magoli 2-2 dhidi ya
Jamhuri ya Czech.
Kufuatia
kitendo hicho EUFA itakaa kikao cha nidhamu hii leo baada ya kupata
ripoti ya refa Mark Clatternburg kuhusina na tukio hilo, wachezaji wa
Croatia wanahofia kuwa timu yao huenda ikaondolewa kwenye michuano
hiyo.
Croatia
walikuwa wanaongoza kwa magoli 2-1 wakati urushaji fataki hizo
uwanjani uliofanywa kwa kupangwa na mashabiki ulipoanza, wachezaji
walijaribu kuwasihi wasifanye hivyo lakini mashabiki wao hawakusikia
na badala yake waliwarushia vitu.
Wachezaji wa Croatia wakijaribu kuwasihi bila ya mafanikio mashabiki wao kuacha kurusha fataki uwanjani
Mmoja wa wasimamizi wa uwanja akielekea kuanguka chini baada ya fataki kulipuka karibu yake
Mashabiki wa Croatia wakidundana ngumi uwanjani wakati wa ghasia hizo




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni