Mabingwa
mara mbili wa kombe la Euro timu ya Hispania wamesonga mbele hatua ya
16 bora, kwa kusakata kabumbu safi dhidi ya wachovu Uturuki katika
mchezo ulioishia kwa ushindi wa magoli 3-0, huko Nice, Ufaransa.
Kwa
rekodi za michuano hiyo ya Euro 2016, Hispania imekuwa timu ya kwanza
kufunga magoli zaidi ya mara mbili. Katika mchezo huo Alvaro Morata
aliipatia Hispania goli la kwanza na Nalito kuongeza la pili kisha
Morata kumalizia la tatu.
Cesc Fabregas akidhibitiwa vilivyo na wachezaji wa Uturuki
Nalito akiwa ameupachika mpira wavuni na kumpoteza maboya kipa wa Uturuki



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni