Mke wa rais wa Marekani, Michelle
Obama, pamoja na mabinti wake wametua nchini Morocco katika ziara yao
ya siku sita kuhamasisha elimu Afrika na kukaribishwa na mke wa
Mfalme Mohammed VI, Princess Lalla Selma katika uwanja wa ndege.
Michelle na familia yake wametua
kwenye uwanja wa Menara Jijini Marrakesh leo baada ya kukaa siku moja
nchini Liberia jana katika kambi ya viongozi wasichana na kuwasihi
watoto wakike katika taifa hilo masikini duniani kutoacha elimu.
Malia Obama akisalimiana na Princess Lalla Selma
Princess Lalla Selma akiwatambulisha maafisa wa Morocco kwa Michelle Obama
Michelle Obama akiwa na rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni