.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 16 Juni 2016

MWILI WA MTOTO ALIYECHUKULIWA NA MAMBA WAPATIKANA FLORIDA

Polisi waliokuwa wakimtafuta mtoto wa kiume aliyevutwa majini na mamba katika eneo la Walt Disney World huko Florida wamefanikiwa kuupata mwili wake.

Wazamiaji wamefanikiwa kuukuta mwili huo wa mtoto huyo wa miaka miwili ukiwa kamili na kuutoa chini ya kina cha maji na kuuonyesha kwa familia yake.

Mkuu wa polisi wa kaunti ya Orange, Jerry Demings, amesema jina la mtoto huyo aliyetoweka tangu avutwe na mamba kwenye maji ni Lane Graves anayetokea huko Nebraska.

Tangu shambulio hilo mamba watano walipatikana na kuuwawa katika eneo hilo wakati wa kumtafuta mtoto huyo.
               Picha za eneo la maji ambalo limewekwa tahadhari kuonyesha kuna mamba
             Fukwe nazo zilifungwa ili kuepusha maafa baada ya kubainika kuwapo mamba

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni